Maamuzi ya jeshi la Polisi baada ya huyu Askari wa Tanga aliyenaswa kwenye video
Novemba 9, 2015
kulikuwa na headlines kwenye mitandao mbalimbali baada ya video
kusambazwa na wasiojulikana ikimuonyesha Askari wa usalama wa barabarani
Anthony Temu kutoka kituo cha polisi Kabuku Tanga akichukua rushwa kutoka kwenye gari alilolisimamisha.
Baada ya hii taarifa kusambazwa
mitandaoni kamanda wa polisi mkoani Tanga, Zuberi Mwombeji amethibitisha
hii ishu nzima kutokea na kwamba Temu alihojiwa na kukiri kwamba ni
kweli alifanya hivyo, baada ya hapo Kamanda Mwombeji amesema
wamemkabidhi kwa TAKUKURU.
‘Tumechunguza taarifa zile na
tumemtafuta tumemshughulikia na kumkabidhi kwa maafisa wa TAKUKURU
wanaendelea na uchunguzi sababu wao ndio wanashughulika na maswala haya
ya rushwa‘ – Kamanda Mwombeji.
No comments:
Post a Comment