Friday, November 6, 2015

Barnaba katuletea mrembo mwingine Bongo Flevani… anaitwa Kleyah (Msobe Msobe Feat. Barnaba)

Staa wa Bongo Fleva, Barnaba ni mmoja ya mastaa wachache ambao ni waandishi wazuri wa nyimbo na ameandika ngoma nyingi sana ambazo zimeimbwa na mastaa wengine kama akina Vee Money, Shilole, na wengine wengi.
Barnaba Classic kaona atutambulishie mrembo mwingine, jina lake ni Kleyah… Mrembo huyu kaamua kuufuata muziki lakini kwa sasa bado ni mwanafunzi anayetarajia kupata Degree ya mambo ya Utawala wa Kimataifa (Master’s degree in International Management) mwaka 2016 Chuo cha Phoenix, Marekani.
Barnaba IIMdundo unaomtambulisha ndio huu ‘Msobe Msobe‘.. kazi ya mikono ya Barnaba Classic mwenye pale kwenye studio anayoimiliki.

No comments:

Post a Comment