Friday, November 6, 2015

Misri yazuia ndege za shirika la Uingereza



 Watu wengi tayari wamefika uwanja wa ndege
Serikali ya Misri imesimamisha safari za shirika la ndege la Easyjet ambalo lilikuwa limepangiwa kuwasafirisha baadhi ya Waingereza waliokwama mji wa Sharm el-Sheikh leo.
Ndege za shirika la Easyjet pamoja na ndege za mashirika ya Monarch, Thomson na British Airways ndizo zilizokuwa zimepangiwa kuwasafirisha Waingereza waliokuwa Sharm el-Sheikh baada ya Uingereza kusitisha safari za ndege za kuingia na kutoka mji wa Sharm el-Sheikh Jumatano.
Hii ni baada ya kuibuka kwa uwezekano kwamba huenda ndege ya Urusi iliyoanguka baada ya kupaa kutoka mji huo Jumamosi iliyopita ikiwa na abiria 224 ililipuliwa.
Taarifa hizo zimeshutumiwa na Urusi na Misri.
Maafisa wa Easyjet wamesema maafisa wa Misri hawakubali ndege za Uingereza zitue katika uwanja huo wa ndege.
Ndege mbili za shirika hilo zilizokuwa zimepangiwa kuondoka kutoka viwanja vya ndege vya Gatwick na Luton nchini Uingereza bado zitaondoka kama zilivyopangiwa.
Lakini maafisa wa Easyjet wamesema ndege nyingine zinazopanga kuondoka kutoka Uingereza kwenza Sharm el-Sheikh kuwachukua abiria hazitaweza kuhudumu.

No comments:

Post a Comment