Magufuli aagizwa kumaliza mgogoro Zanzibar
Marekani imeitaka serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya raia wa Zanzibar katika uchaguzi wa urais uliopita.
Akimtumia
risala za pongezi rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa ushindi
wake wa uchaguzi mkuu uliopita, waziri wa maswala ya kigeni nchini humo
John Kerry amesema kuwa Marekani inaendelea kukerwa na hatua ya
kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo.
''Tunautaka utawala mpya kuhakikisha kuwa maamuzi ya raia wa Zanzibar yanazingatiwa na kuheshimiwa'',alisema.
Amesisitiza
wito wa Marekani wa kutofutiliwa mbali kwa matokeo hayo huku akizitaka
pande zote kushirikiana kwa lengo la kufanikisha mchakato huo wa
kidemokrasia kwa uwazi na amani.
Wakati huohuo waziri huyo amempongeza rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kufanikisha uchaguzi mkuu uliopita.
No comments:
Post a Comment