Toilet Cafe? Yes.. hii ndio Moscow, kiti, bakuli vyote kwenye umbile la choo Mgahawani..
Nyumba nyingi huwezi kukutana na jiko
lililo karibu kabisa na choo, kwa sababu hata matumizi ya sehemu hizo
mbili yako tofauti… vipi hii ya jiko na choo kwenye chumba kimoja je?
Kwenye vitu ambavyo vimenishtua leo na hii imo, yani watu wa Moscow Urusi wameona haja ya kuweka mambo tofauti… bango tu linalotangaza biashara limeandikwa Crazy Toilet Cafe,
mgahawa ambao usishangae ukaagiza supu na ikaletwa ndani ya bakuli
linalofanana na sinki la choo.. kuanzia kiti cha kukalia kina umbile
hilo, mpaka mabakuli ya chakula na vyombo vingine viko hivyo !!
Mgahawa wa aina hii ni wa kwanza kwa nchi za Ulaya, lakini unaambiwa hata Taiwan nako uko mgahawa ambao vitu vyake vya ndani vinafanana na sinki la chooni !!
Kila mtu anakaribishwa kwa huduma poa za
msosi, na bei ni ya kawaida kabisa kwa hiyo sio mahali pa kupaogopa…
mfano ukafunguliwa mgahawa wa hivi Bongo utatamani kwenda na mtu wako
mkaenjoy lunch?
Hii hapa video ya Mgahawa wa Crazy Toilet Cafe uliofunguliwa Moscow, Russia..
Kama hukuwahi kuijua ya mgahawa wa hivyo Taiwan nayo hii hapa mtu wangu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa
na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK
ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo
kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa
No comments:
Post a Comment