CCM imefanikisha kunyakua viti 64 maalum,Chadema 36
CCM kimejipatia viti 64, huku CHADEMA kijipatia viti 36 kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Chama cha Upinzani CUF nacho kimejipatia viti 10.
Akizungumza
na waandishi wa habari,jaji Damian Lubuva aidha amesema kuwa idadi ya
viti maalum vya wabunge wanawake imepanda hadi kufikia 40.
Amesema kutokana na
uchaguzi huo CCM ilipata kura za ubunge milioni 8,333,953, huku CHADEMA
ikipata kura 4,627,923 nayo CUF ikipata kura 1,257,051.
Jaji
lubuva amesema kuwa kutokana na majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi
,mgawanyo wa viti maalum sasa ni 110 ambapo viti vitatu vilivyosalia
vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.
No comments:
Post a Comment