Mamba kulinda wafungwa hatari Indonesia
Mkuu wa shirika la kupambana na dawa za kulevya Indonesia amependekeza mamba watumiwe kulinda wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.
Budi
Waseso anataka taifa hilo lijenge gereza kwenye kisiwa na kizingirwe na
mamba akisema wanyama hao ni walinzi bora kushinda wanadamu, kwani
hawawezi kuhongwa.
Amesema atazuru maeneo mbalimbali katika taifa hilo kutafuta mamba wakali zaidi.
Indonesia
ina moja ya sheria kali zaidi za kupambana na dawa za kulevya duniani
na ilianza tena kunyonga watu baada ya kusitisha hukumu hiyo kwa miaka
mine 2013.
"Tutaweka mamba wengi sana huko,” Bw Waseso alinukuliwa na tovuti moja nchini humo kwa jina Tempo.
"Huwezi kuwahonga mamba. Huwezi kuwashawishi waruhusu washukiwa watoroke.”
Mpango
huu bado umo katika hatua za mwanzo mwanzo nab ado haijaamuliwa gereza
hilo litakuwa wapi na ni lini litafunguliwa, shirika la habari la AFP
limesema.
No comments:
Post a Comment