Wapenzi wa jinsia moja watoroka Uganda
Mamia ya watu wa jamii ya jinsia moja nchini Uganda wamelitoroka taifa hilo ili kukwepa ubaguzi na mateso.
Lakini sasa wamekwama nchini Kenya ambapo hali sio shwari.
Mwandishi
wa BBC Emmanuel Igunza alisafiri hadi katika kambi moja ya wakimbizi
ambapo vijikaratasi vilichapishwa katika kuta vikiwataka wakaazi
kutojichanganya na watu wa jinsia hiyo.
Raia hao wa Uganda wamepiga kambi huko Kakuma kutoka taifa lenye amani.
Wakaazi wengine waliopo katika kambi hiyo wanatoka katika maeneo yaliyokumbwa na migogoro kama vile Sudan Kusini na Somalia.
No comments:
Post a Comment