Wednesday, November 4, 2015

Mifuko ya magari yaua watu saba

Mifuko hiyo airbag ikishonwa
Mamlaka ya usalama nchini Marekani wamependekeza kampuni ya Takata ya Japan, inayotengeneza mifuko ya usalama garini maarufu kama airbag kupigwa faini ya zaidi ya dola za kimarekani milioni mbili baada ya mifuko hiyo kusababisha vifo vya watu saba .
Katika kile kinachoelezwa kama adhabu kubwa na ngumu kuwahi kutolewa kwa kampuni ya utengenezaji magari na vifaa vyake.

Takata waliamriwa kulipa pesa tasilimu dola milioni sabini mara moja lakini pia huenda Takata wakakabiliwa na faini nyingine ya dola za kimarekani milioni moja na thelathini endapo wataendelea kutumia mchanganyiko wa malighafi unaosababisha mifuko hiyo ya usalama.
Karibu magari milioni thelathini na nne yaliyoko nchini Marekani yamevumbua hitilafu hiyo mapema mwaka huu.
Katibu mkuu wa masuala ya usafiri nchini Marekani,Anthony Fox amesema kwamba kampuni hiyo ya Takata imekataa kukubali kuwa mifuko hiyo ya kiusalama si salama kwa miaka kadhaa sasa ,na kugeuka kuwa mgogoro mkubwa wa usalama garini .

No comments:

Post a Comment