Wednesday, November 4, 2015

Ndege yaanguka Sudan Kusini


Watu kadha wanahofiwa kufariki baada ya ndege iliyotengenezewa Urusi kuanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Juba, Sudan Kusini.
Ripoti zinasema huenda watu 40 wamefariki, baadhi wakiwa watu walioangukiwa na ndege hiyo ardhini.
Ndege hiyo ilianguka kwenye ukingo wa mashariki wa Mto Nile.
Maafisa wanatafuta manusura.
Msemaji wa rais Ateny Wek Ateny ameambia shirika la habari la Reuters kwamba mhudumu mmoja na mtoto, ambao walikuwa kwenye ndege hiyo, wamenusurika.

No comments:

Post a Comment