Mkurugenzi wa MTN ajiuzulu kufuatia faini Nigeria
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya simu ya MTN amejiuzulu kufuatia faini kubwa ya dola bilioni 5.2 iliyotozwa na Nigeria
Mkuu
huyo wa kampuni hiyo kubwa zaidi barani Afrika Sifiso
Dabengwa,aliwasilisha barua ya kujiuzulu mara moja kwa maslahi ya wenye
hisa na uendelevu wa kampuni hiyo.
Faini hiyo iliyotozwa na tume
ya mawasiliano ya Nigeria kufuatia utepetevu wa MTN ya kukataa kuzima
nambari za simu ambazo hazijasajiliwa kwa mujibu wa kanuni mpya za taifa
hilo.
MTN ilipewa majuma mawili pekee kuwa imelipa faini hiyo kubwa inayotoshana na faida iliyopata mwaka uliopita.
MTN ina hadi tarehe 16 Novemba kuwa imelipa faini hiyo ya dola 5.2.
Dabengwa
aliandika ''kufuatia faini kubwa iliyotozwa MTN Nigeria ,kwa niaba
yangu na wenye hisa wa kampuni hii nimeamua kujiuzulu mara moja''
Dabengwa amekuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo tangu mwaka wa 2011.
Phuthuma Nhleko amechaguliwa kuwa kaimu mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi 6.
Inadhaniwa kuwa serikali ya Nigeria ilichukua hatua
kali za kinidhamu dhidi ya MTN kufuatia utekaji nyara wa aliyekuwa
waziri wa zamani wa fedha Chifu Olu Falae.
Waliomteka nyara walitumia simu ambayo haijasajiliwa ya MTN kuitisha malipo ya kumkomboa Nigeria ndio mteja mkubwa zaidi wa kampuni hiyo yenye asili ya Afrika Kusini ikiwa na wateja milioni 28.5.
Soko la pili kwa ukubwa kwa MTN ni Iran na kisha Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment