TP Mazembe mabingwa wa Afrika
Klabu ya soka ya TP Mazembe, ya Jamuhuri ya Kidemocrasia ya Congo imetwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika.
TP
Mazembe wakicheza kwao katika uwanja wa Stade du TP Mazembe Lubumbashi,
waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi Union Sportive Medina d’Alger.
Mshambuliaji
Mbwana Samatta ndiye aliyeanza kuifungia timu yake bao la kwanza kwa
mkwaju wa penalti katika dakika ya 75 ya mchezo, kisha Roger Assale
akahitimisha kazi kwa bao la pili katika dakika ya 90.
Mazembe
imenyakua Ubingwa huu wa Afrika, ikiwa ni mara yao ya 5, kwa jumla ya
Mabao 4-1 baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali
ya kwanza uliofanyika wiki iliyopita.
Bao la Samatta katika mchezo huo, limemfanya afikishe bao 7 msimu huu na kuibuka ndie mfungaji bora wa michuano hii.
Baada
ya kutwaa taji hili, TP Mazembe wamezoa donge la dola 1.5 milioni na
pia wataiwakilisha Afrika kwenye mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa
Duniani huko Japan mwezi Desemba.
No comments:
Post a Comment