Wednesday, November 4, 2015

Museveni asema ana imani atashinda urais

Juhudi za Mbabazi na Besigye kutaka kuafikiana mmoja wao ashindane na Museveni zimegonga mwamba
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema wagombea urais wanaoshindana naye kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao si tishio kwake.
“Hiki hakitakuwa kinyang’anyiro kikali,” ameambia kikao cha wanahabari mjini Kampala.
Wapinzani wakuu wa Bw Museveni wanatarajiwa kuwa Amama Mbabazi na Kizza Besigye, ambao walikuwa marafiki wake wakuu wakati mmoja.


"Nasikia watu wakizungumza kuhusu kupiga vita ufisadi. Utawezaje kukabiliana na ufisadi ilhali twasikia ukiomba huyu na yule wajiunge nawe?” amesema.
"Lazima uwe na uwezo,” ameongeza Bw Museveni.
Hii ni mara ya kwanza kwa Bw Mbabazi, aliyekuwa waziri mkuu wakati mmoja, kuwania urais.
Bw Museveni ameongoza Uganda tangu 1986.
Museveni aliwasilisha karatasi za uteuzi kwa tume ya uchaguzi jana
Tume ya uchaguzi ya Uganda imeidhinisha watu wanane kuwania urais mwaka ujao wakiwemo Bw Museveni, Bw Besigye, Bw Mbabazi na Venansius Baryamureba.
Kampeni zitaanza Novemba 9.

No comments:

Post a Comment