Mwanafunzi ‘aiba’ basi ili asikose mtihani
Mwanafunzi mmoja wa shule ya upili Afrika Kusini aliiba basi na kulitumia kufika shuleni ili asikose mtihani wa somo la hesabu.
Ajabu ni kwamba, mwanafunzi huyo amesema hakuwahi kuendesha basi kabla ya kisa hicho.
"Hapana, ni gari tu la kawaida," Le-Aan Adonis ameambia wanahabari.
Mwanafunzi
huyo wa umri wa miaka 21 pamoja na wenzake, waliachwa wamekwama
kijijini mkoa wa Western Cape baada ya dereva wa basi aliyefaa
kuwasafirisha umbali wa kilomita 30 kugoma na kutofika kazini.
Kijana huyo, baada ya kuona funguo za gari zilikuwa zimeachwa ndani ya basi, aliamua kulichukua, kuwa dereva na kuliendesha.
Lakini
alisimamishwa na afisa wa trafiki na kupigwa faini ya $360 (£236) kwa
kuendesha basi bila leseni na bila cheti cha kuendesha magari ya umma.
Alipoulizwa
atalipaje faini hiyo, alijibu: “Wazazi wangu hawana pesa, hivyo iwapo
kuna mtu anaweza kunisaidia kulipa faini hiyo, nitashukuru sana.”
Alijipata
taabani, lakini kwa wanafunzi wenzake yeye ni shujaa kwani ilikuwa
muhimu sana kwao kufanya mtihani huo wa kumaliza shule, na
hawakuchelewa.
No comments:
Post a Comment