Thursday, November 5, 2015


Rais JK, Seif wakubaliana, Dk. John Magufuli kuapishwa leo, UKAWA, CHADEMA wakataa kushiriki.

Kikwete, Seif wakubaliana wateta kwa saa moja Ikulu Dar es salaam, Dk. John Magufuli kuapishwa leo, CHADEMA, UKAWA wakataa kushiriki, Rais Kikwete atangaza leo kuwa sikukuu ya mapumziko lakini NECTA inasema sikukuu ya leo haiwahusu kidato cha nne.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli anategemea kuapishwa leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam baada ya kushinda kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika siku ya October 25 2015 na baadhi ya viongozi wa nchi watakaokuwepo leo kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais Mteule ni pamoja na viongozi kutoka Uholanzi, Marekani, Uingereza, Nigeria na Misri.
Aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa jimbo la Iringa mjini, Frederick Mwakalebela ameenda Mahakamani kupinga matokeo ya Ubunge ya jimbo hilo dhidi ya Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMARwanda wataka Sheria zitafsiriwe kwa Kiswahili, lugha inayotumiwa zaidi na nchi za Umoja wa Africa Mashariki, EAC.
Mgombea Urais Zanzibar, Maalim Seif jana alikutana na Rais Jakaya Kikwete na kufanya mazungumzo ya saa moja juu ya hali ya kisiasa visiwani Zanzibar, taarifa iliyotolewa na Ikulu jana imesema kuwa Maalim Seif na Rais Kikwete wamekubaliana kuwa kila pande iendele kutafuta suluhisho juu ya hali ya kisiasa inayoendelea visiwani humo.

No comments:

Post a Comment