Majeshi ya upinzani yateka eneo Syria
Wizara ya ulinzi ya
Marekani imesema kwamba wanajeshi wa upinzani waliounda kundi lao hivi
karibuni nchini Syria,wamefanikiwa kutwaa eneo lenye ukubwa wa kilomita
mia mbili katika mapambano yake na kikundi cha kigaidi cha Islamic State
upande wa kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa wizara
hiyo ya ulinzi aliyeko mjini Baghdad,Steve Warren,ameelezea kuwa
mapambano hayo yanayoendelea karibu na mji wa Al-Hawl yanahusisha maelfu
ya wapiganaji wa upande wa upinzani ambao wameongezewa nguvu na askari
wa angani wa majeshi washirika ya Marekani.Kikundi hicho kinachojiita jeshi la Syria lenye muungano wa nchi za Kiarab,kimekuwa kikitoa ahadi ambapo mpango mpya wa nchi ya Marekani wenye lengo la kupambana na kikundi hicho cha wanamgambo wa Islamic State walioko nchini Syria.
No comments:
Post a Comment