Chris Brown kuzuiliwa tena kufanya tour Australia?! New Zealand, Canada na Britain je?
Mwezi September mwaka huu, ilionekana vigumu kwa staa wa muziki wa R&B, Chris Brown kuingia Australia
na kufanya show, sababu kuu zilikuwa mbili, utapeli na historia yake ya
kupiga wanawake… lakini hiyo ilikuwa issue ya miezi mitatu iliyopita.. December hii mambo yapoje?
Serikali ya Australia
imempatia staa huyo wa Virginia notice kuhusu kufikiria kuingia nchini
humo, notice ambayo akiichukulia poa itamzuia kufanya tour yoyote Australia… Kufuatia notice hiyo, promter wa Chris Brown hivi karibuni alichukua maamuzi ya kufuta tour mbili za msanii huyo, Tour ya Australia na tour nyingine ya New Zealand!
Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard wa Marekani, promoter wa Chris Brown alichukwa time na kusema…
>>> “Mr.
Brown na mapromoter wake wote wanamatumaini kuwa tour hizo zitafanyika
siku zijazo za mbele, licha ya hayo Mr. Brown angependa kuchua nafasi
hii kuomba radhi kwa mashabiki wake na pia kuwashukuru kwa support yao
kubwa wanayompa na anategemea kukutana na nyie kwenye tour nyingine
zijazo“. <<< Nukuu kutoka Billboard.
Sababu kuu ya kumzuia Chris Brown
kuingia kwenye nchi hizo na kufanya tour ni zile zinazoambatana na
historia yake ya kumpiga na kumjeruhi aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Rihanna… ukiacha hayo Britain, Canada na New Zealand pia wamegoma kutoa visa yoyote kwa ajili ya msanii huyo kuingia kwenye nchi hizo.
No comments:
Post a Comment