Thursday, December 3, 2015

Huu ni mpango wa Wema Sepetu kwa mwaka 2016


Mwaka 2015 unakaribia kuisha na baadhi ya watu wameshaanza kufanya mipango yao kwa mwaka 2016. Kwa mwaka 2015 Wema Sepetu ametajwa mara kadhaa kutokua na maelewano na baadhi ya marafiki zake wa zamani kama Kajala, pia kuendeleza uhusiano mzuri na watu aliokua hapatani nao zamani kama Penny.
Kwenye moja ya mipango ya Wema Sepetu kwa mwaka 2016 ameweka wazi kwamba yeye hana mpango wa kuanza mwaka akiwa na beef na mtu yoyote. Wema amesisitiza kwamba anaomba watu wote aliowakosea kwa mwaka 2015 wamsamehe na yeye anawasamehe wote waliomkosea.
Maneno ya Wema Sepetu kuhusu mpango huo yapo hivi, “Mi nataka mwaka unapoanza inshallah tukijaaliwa nisiwe na beef na mtu yoyote wala kiumbe yoyote… Kwa wale nilowakosea na walionikosea …. Nasema Im sorry….. Life Goes On…. We all live to make mistakes…. Ama nene….  And I thank everyone for making me the person Iam TODAY….”

No comments:

Post a Comment