Huduma ya taifa' Eritrea ni dhalimu
Shirika la
kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International, limetaka
jamii ya kimataifa kutambua shughuli ya serikali ya Eritrea kuwaigiza
raia wake kwa nguvu katika huduma ya tiafa, kama ukiukaji wa haki za
binadamu.
Shirika hili linasema hatua hii ya serikali inachochea tatizo la ongezeko la wakimbizi duniani.
Kwenye
ripoti yake, Amnesty International inasema maelfu ya vijana wa Eritrea
wanaikimbia nchi na kutafuta hifadhi Ulaya ili kuepuka kuingizwa kwenye
huduma ya taifa.
Baadhi ya raia wa Eritrea
waliokimbia nchini waliambia shirika hilo kwamba waliojaribu kukimbia
kutoka huduma hiyo hupata adhabu kali.
Eritrea imejitetea dhidi ya
madai kwamba inatumia huduma hii kuwadhulumu raia wake na kusema
wakosoaji wa mpango huo wanaingilia uhuru wake na kuhujumu maendeleo.
No comments:
Post a Comment