Kidum na maisha mapya ya wokovu, sasa hivi ni yeye na Mungu tu!
Msanii wa muziki kutoka Kenya mwenye asili ya Burundi, Kidum anazikamata headlines za leo baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo mwenye hit single ya Namba Moja amemgeukia Mungu na kuamua kuokoka!
Nimekutana na stori kwenye mtandao wa The Citizen inayosema siku ya jumatatu wiki hii Mchungaji ajulikanae kwa jina la Eric Omba alichukua time na kushare na watu wake kupitia page yake ya Instagram picha zake akiwa anambatiza msanii huyo na kuandika caption ya maneno inayosema…
>>> “Baada
ya kuokoka, Kidum sasa ameamua kusimama kwenye uwokovu kwa kumgeukia
Yesu Kristo. Nina furaha kubwa sana kama mchungaji aliyepata fursa ya
kumbatiza upya kaka yangu. Amekiri mbele ya dunia nzima kuwa Yesu ni
mwokozi wa maisha yake.” <<< nukuu kutoka mtandao wa The Citizen.
Kidum ameshafanya kazi kadhaa za Gospel ikiwa pamoja na kuachia nyimbo kama Mungu Anaweza na Kimbia ila sasa amerudi upya kumtumikia Mungu kwa levo ya juu zaidi.
Ukiacha mbali kazi zake za Gospel, Kidum pia alifanikiwa kutoa hit singles kadhaa kama Haturudi Nyuma ngoma aliyoshirikisha Juliana msanii kutoka Uganda na Nitafanya.
Historia ya Kidum kwenye kurasa za burudani ilianza mwaka 1995 alipoenda Kenya kunusuru maisha yake kutokana na hali ya kisiasa iliyokuwa inaendelea Burundi na toka kipindi hicho Kidum aliweza kujitengenezea jina kama msanii wa muziki Kenya, ambapo alipata pia fursa ya kusafiri nchi mbalimbali kutangaza muziki wake.
Hizi ni baadhi ya picha za ubatizo wa Kidum nilizofanikiwa kuzinasa:
No comments:
Post a Comment